LEO 14.09. 2025 NI DOMINIKA YA KUTUKUZWA KWA MSALABA, MWAKA C.
MATAYARISHO YA LITURUJIA
- Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, ni Dominika ya 25 Kipindi cha kawaida, Mwaka C. Misa hapa Kanisani zitakuwa saa moja asubuhi, saa tatu kasorobo na saa nne unusu asubuhi.
MISA WIKI HII
- Wanajumuiya wa Mary Help of Christians, watakuwa na Misa, Alhamisi ijayo, tarehe 18 Septemba, hapa Kanisani, kuanzia saa kumi na mbili jioni.
MATANGAZO MENGINE
- Wanachama wa kundi la Divine Mercy wanafahamishwa kwamba kutakuwa na mafunzo leo Kanisani St. Patrick’s, kuanzia saa nane mchana. Wanaombwa kuleta Bibilia zao.
- Wasimamizi wa St. Patrick’s Self Help Group, wanawaalika wanachama kwa siku ya mafunzo na uhamasishaji Jumamosi ijayo, tarehe 20 Septemba, katika ukumbi wa Kanisa la St. Patrick’s, kuanzia saa tatu asubuhi.
- Afya Care Limited itakuwa na uchunguzi wa bure wa magonjwa mbalimabli Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, hapa Kanisani, baada ya Kila Misa.
- Wanachama wa CWA wanafahamishwa kwamba watakuwa na mafundisho tayarishi Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, hapa Kanisani, kuanzia saa sita mchana.
TANGAZO LA NDOA MARA YA PILI
- Tunatangaza nia ya ndoa takatifu kati ya Patrick Wanjohi, mwanaye Susan Nyawira, kutoka Mekaro, Nyandarua, akifunga ndoa na Purity Karendi, bintiye George Ndiga na Justa Mukwaiti, kutoka Mpiani, Tharaka-Nithi.
Kama kuna mtu ana kizuizi kuhusu ndoa hii ajulishe Ofisi ya Parokia.





