FEAST OF THE EXALTATION OF THE CROSS, YEAR C.

LEO 14.09. 2025 NI DOMINIKA YA KUTUKUZWA KWA MSALABA,  MWAKA C.

MATAYARISHO YA LITURUJIA

  • Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, ni Dominika ya 25 Kipindi cha kawaida, Mwaka C. Misa hapa Kanisani zitahudumiwa kama ifuatavyo:
  • 6:45 am Wanachama wa Haki & Amani na Legio Maria.
  • 8:15 am Watumishi wa Misa.
  • 10:00 am PMC na MYM Animators.
  • 11:45 am Wanachama wa CMA.

MISA WIKI HII

  • Wanajumuiya wa Mtakatifu Cyprian, Mtaa wa Government Quarters, watakuwa na Misa, Jumatano ijayo, tarehe 17 Septemba, kuanzia saa moja jioni.
  • Wanajumuiya wa Mtakatifu Matthew, Mtaa wa Government Quarters, watakuwa na Misa, Ijumaa ijayo, tarehe 19 Septemba, kuanzia saa moja jioni.

MATANGAZO MENGINE

  • Wanachama wa kundi la Divine Mercy wanafahamishwa kwamba kutakuwa na mafunzo leo hapa Kanisani, kuanzia saa nane mchana. Wanaombwa kuleta Bibilia zao.
  • Wasimamizi wa St. Patrick’s Self Help Group, wanawaalika wanachama kwa siku ya mafunzo na uhamasishaji Jumamosi ijayo, tarehe 20 Septemba, katika ukumbi wa Kanisa, kuanzia saa tatu asubuhi.
  • Wanachama wa CWA wanafahamishwa kwamba watakuwa na mafundisho tayarishi Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, katika Kanisa la Mtakatifu Petro Mwamba, kuanzia saa sita mchana.

TANGAZO LA NDOA MARA YA PILI

  • Tunatangaza nia ya ndoa takatifu kati ya Patrick Wanjohi, mwanaye Susan Nyawira, kutoka Mekaro, Nyandarua, akifunga ndoa na Purity Karendi, bintiye George Ndiga na Justa Mukwaiti, kutoka Mpiani, Tharaka-Nithi.
  • Kama kuna mtu ana kizuizi kuhusu ndoa hii ajulishe Ofisi ya Parokia.

LEO 19. 01. 2025 NI DOMINIKA YA PILI MWAKA C.

  • Tunawashukuru wote waliotoa zaka Jumapili iliyopita. Tunaomba baraka za Mungu ziwe nanyi na familia zenu. Mungu awazidishie kwa wingi kile mnachomtolea kwa furaha na upendo.

MATAYARISHO YA LITURUJIA

  • Tunatoa shukurani za dhati kwa kila mmoja wenu kwa kuungana nasi katika Misa za Jumapili iliyopita. Kuweko kwenu katika nyumba ya Bwana, kunaleta furaha kubwa na kunatia nguvu katika safari yetu ya kiroho.
  • Jumapili ijayo, tarehe 26 Januari, ni Dominika ya Tatu Mwaka C. Misa hapa Kanisani zitahudumiwa kama ifuatavyo:
  • 6:45 am Wanachama wa Young Catholic Adults.
  • 8:15 am Wanachama wa Catholic Teachers Association.
  • 10:00 am      Beacon Boys.
  • 11:45 am Kwaya ya Mtakatifu Theophilus.

MISA WIKI HII

  • Wanajumuiya wa Mtakatifu Agnes, Mtaa wa Ziwani, watakuwa na Misa, Jumatano ijayo, tarehe 22 Januari, nyumbani kwake John Njoroge, nyumba nambari 590, kuanzia saa moja jioni.

MATANGAZO MENGINE

  • Leo, kuna mkutano wa Baraza la Kichungaji la Parokia (Parish Pastoral Council) hapa Kanisani, kuanzia saa nane.
  • Padre atawatembelea wagonjwa na wakongwe Ijumaa ijayo, tarehe 24 Januari, kuanzia saa tatu asubuhi.
  • Wanachama wa CWA, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na semina na Misa, Jumamosi ijayo, tarehe 25 Januari, hapa Kanisani, kuanzia saa moja unusu asubuhi.
  • Viongozi wale watano (Executive) wa Parokia, kutoka vikundi vyote vya Kanisa, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na mkutano, Jumapili ijayo, tarehe 26 Januari, hapa Kanisani, kuanzia saa nane.
  • Wakristo ambao wangependa kujifunza Kenya Sign Language wanaombwa kujisajili katika ofisi ya Parokia, ifikapo Ijumaa, tarehe 31 Januari.
  • Ifuatayo ni orodha ya vikundi vya Kanisa na Padre msmamizi:
  • CMA/Beacon Boys
  • PMC
  • MYM
  • CJPD
  • Kwaya/Liturujia

Rev. Fr. Bernard Kabiu

  • YSC
  • Moyo Mtakatifu wa Yesu
  • Pioneer
  • CPA
  • CTA

Rev. Fr. James Mwaura

  • CWA
  • YCA
  • Anne & Joachim
  • Legio Maria

        Rev. Fr. Elijah Kinyua

LEO 18. 08. 2024 NI DOMINIKA YA 20 MWAKA B.

  • Tungependa kuwashukuru wote waliotoa zaka zao Jumapili iliyopita. Kwa ukarimu wenu, tumebarikiwa na tunaweza kuendeleza huduma mbalimbali za Kanisa letu na Parokia yetu. Asanteni sana na Mungu awabariki.

MATAYARISHO YA LITURUJIA

  • Tunatoa shukurani za dhati kwa nyote mliohudhuria Misa za Jumapili iliyopita na kwa michango yenu. Uwepo wenu na kujitoa kwenu, vimekuwa baraka kubwa kwa Kanisa letu.
  • Jumapili ijayo, tarehe 25 Agosti, ni Dominika ya 21 Mwaka B. Misa hapa Kanisani zitahudumiwa kama ifuatavyo:
  • 6:45 am Mtaa wa Majengo.
  • 8:15 am Mtaa wa UTI.
  • 10:30 am Mtaa wa Starehe.
  • 11:45 am Mtaa wa Ofafa.

MISA WIKI HII

  • Wanajumuiya wa Mtakatifu Hellen, Mtaa wa Bahati, watakuwa na Misa, Jumanne ijayo, tarehe 20 Agosti, nyumbani kwake Freshia Njoki (Mathee) ploti nambari 4, kuanzia saa moja jioni.

MATANGAZO MENGINE

  • Wanajumuiya kutoka Mitaa ya Bahati, Majengo, na Government Quarters, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na maombi ya pamoja leo, mahali kwaya hukutana, kuanzia saa nane.
  • Wanachama wote wa CMA , wanafahamishwa kwamba, mazoezi ya tamasha ya muziki, ni kila Jumapili, huko Witeithie Carpark, kuanzia saa nane.
  • Padre John Njenga, atakuwa likizo ya kila mwaka kuanzia tarehe 19 Agosti hadi tarehe 21 Septemba.
  • Watoto wa PMC watakuwa na mzunguko wa Rozari Takatifu, Jumanne ijayo, tarehe 20 Agosti, katika Mtaa wa Ofafa, kuanzia saa kumi na mbili jioni.
  • Wanachama wa CMA, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na Recollection, Kanisani St. Francis of Assisi, Athena, Jumamosi ijayo, tarehe 24 Agosti, kuanzia saa mbili asubuhi. Wanombwa kujisajili kwa shilingi mia mbili.
  • Wanachama wa CWA, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na mafundisho tayarishi daraja la kwanza na la pili, Jumapili ijayo, tarehe 25 Agosti, Kanisani St. Peter the Rock, kuanzia saa tano unusu asubuhi.
  • Wawakilishi wa Liturjia kutoka kila Jumuiya na kikundi cha Kanisa, wanafahamishwa kwamba watakuwa na mkutano Jumapili ijayo, tarehe 25 Agosti, hapa Kanisani, kuanzia saa tisa.
  • Parokia yetu inakusudia kuanzisha kikundi cha wataalamu wa ushauri. Tunawaomba wajisajili kupitia kwa Catherine Wanjiku, simu nambari 0724891172, au ofisi ya Parokia kufikia Jumamosi, tarehe 31 Agosti.
  • Kikundi cha CMA kinawaalika wanaume ambao wangependa kuwa wanachama kwa mafundisho tayarishi Jumapili tarehe 1 Septemba. Wanaombwa kujisajili kwa Moderator wa CMA.

TANGAZO LA NDOA MARA YA TATU

  • Tunatangaza nia ya ndoa takatifu kati ya Leon Kiarie Ndekei, mwanaye Susan Wairimu Maithai, kutoka Kitusuru, akifunga ndoa na Angela Wangari, bintiye Eng. Joseph Mukora Wakimani, na Emmah Wanjira Mukora, kutoka St. Patrick’s.

 

Kama kuna mtu ana kizuizi kuhusu ndoa hii ajulishe ofisi ya Parokia.

TODAY 14.09.2025 IS THE EXALTATION OF THE CROSS, YEAR C.

MASS ANIMATION

  • Next Sunday, 21 September, is the 25 Sunday in Ordinary Time, Year C. Masses here in Church shall be animated as follows:
  • 6:45 am Members of CJPD and Legion of Mary.
  • 8:15 am Mass Servers.
  • 10:00 am PMC and MYM Animators.
  • 11:45 am Members of CMA.

MASS THIS WEEK

  • Members of St Cyprian SCC, Government Quarters Estate, will celebrate Mass, next Wednesday, 17 September, from 7 pm.
  • Members of St. Matthew SCC, Government Quarters Estate, will celebrate Mass, next Friday, 19 September, from 7pm.

OTHER ANNOUNCEMENTS

  • Members of the Divine Mercy Group are notified that there will be a session today here in Church, at 2 pm. They are requested to bring their Bibles.
  • The Management of St. Patrick’s Self Help Group, invites members to an education and capacity building day next Saturday, 20 September, at the Church hall, from 9 am.
  • Members of CWA are notified that they will have formation class next Sunday, 21 September, at St. Peter the Rock Church, from 12 noon.

MARRIAGE BANN FOR THE SECOND TIME

  • We announce the intended marriage between Patrick Wanjohi, son of Susan Nyawira, from Mekaro, Nyandarua, marrying Purity Karendi, daughter of George Ndiga and Justa Mukwaiti, from Mpiani, Tharaka-Nithi.

Anybody with an impediment regarding this marriage should forward it to the Parish Office.