LEO 23.03.2025 NI DOMINIKA YA TATU YA KWARESIMA, MWAKA C.
MATAYARISHO YA LITURUJIA
- Tunashukuru kila mmoja wenu kwa kuhudhuria Misa za Jumapili iliyopita. Uwepo wenu na ushiriki wenu ulikuwa baraka ya kweli, na tunafurahia kuwa na fursa ya kuungana pamoja katika imani na ibada.
- Jumapili ijayo, tarehe 30 Machi, ni Dominika ya Nne ya Kwaresima, Mwaka C. Misa hapa Kanisani zitakuwa saa moja asubuhi, saa tatu kasorobo asubuhi na saa nne unusu asubuhi.
MATANGAZO MENGINE
- Wanachama wa CMA, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na mafundisho tayarishi leo, hapa Kanisani, baada ya Misa ya kwanza. Wanachama wapya wanakaribishwa.
- Wanachama wa Youth, wanafahamishwa kwamba, watakuwa na mafundisho tayarishi leo, Kanisani St. Helena Rurii, baada ya Misa ya pili. Wanachama wapya wanakaribishwa.
- Kutakuwa na Njia ya Msalaba na Misa, Ijumaa ijayo, tarehe 28 Machi, hapa Kanisani, kuanzia saa kumi unusu jioni.
- Parokia yetu ina nia ya kuweka kamera za C. C. T. V katika uwanja wetu wa kuegesha magari (carpark) pale witeithie. Tungependa kuwaalika wakristo walio na ujuzi huu, kutuma ombi lao (quatation) kupitia kwa barua pepe: holyrosaryparishwiteithie@gmail.com. Au kwa Whatsapp 0708791626.
- Wazazi walio na watoto wachanga na wangependa wabatizwe wanaombwa kuchukua fomu kutoka kwa walimu wa dini. Malipo ya sadaka ya ubatizo yalipwe kupitia kwa Paybill No. 8998990 Account 002025.




