LEO 14.09. 2025 NI DOMINIKA YA KUTUKUZWA KWA MSALABA, MWAKA C.
MATAYARISHO YA LITURUJIA
- Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, ni Dominika ya 25 Kipindi cha kawaida, Mwaka C. Misa hapa Kanisani zitahudumiwa kama ifuatavyo:
- 6:45 am Wanachama wa Haki & Amani na Legio Maria.
- 8:15 am Watumishi wa Misa.
- 10:00 am PMC na MYM Animators.
- 11:45 am Wanachama wa CMA.
MISA WIKI HII
- Wanajumuiya wa Mtakatifu Cyprian, Mtaa wa Government Quarters, watakuwa na Misa, Jumatano ijayo, tarehe 17 Septemba, kuanzia saa moja jioni.
- Wanajumuiya wa Mtakatifu Matthew, Mtaa wa Government Quarters, watakuwa na Misa, Ijumaa ijayo, tarehe 19 Septemba, kuanzia saa moja jioni.
MATANGAZO MENGINE
- Wanachama wa kundi la Divine Mercy wanafahamishwa kwamba kutakuwa na mafunzo leo hapa Kanisani, kuanzia saa nane mchana. Wanaombwa kuleta Bibilia zao.
- Wasimamizi wa St. Patrick’s Self Help Group, wanawaalika wanachama kwa siku ya mafunzo na uhamasishaji Jumamosi ijayo, tarehe 20 Septemba, katika ukumbi wa Kanisa, kuanzia saa tatu asubuhi.
- Wanachama wa CWA wanafahamishwa kwamba watakuwa na mafundisho tayarishi Jumapili ijayo, tarehe 21 Septemba, katika Kanisa la Mtakatifu Petro Mwamba, kuanzia saa sita mchana.
TANGAZO LA NDOA MARA YA PILI
- Tunatangaza nia ya ndoa takatifu kati ya Patrick Wanjohi, mwanaye Susan Nyawira, kutoka Mekaro, Nyandarua, akifunga ndoa na Purity Karendi, bintiye George Ndiga na Justa Mukwaiti, kutoka Mpiani, Tharaka-Nithi.
- Kama kuna mtu ana kizuizi kuhusu ndoa hii ajulishe Ofisi ya Parokia.





